Habari
UKAGUZI WA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
UKAGUZI WA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
Na OR- INKT, DODOMA:
Mwenyekiti wa kamati ya mradi wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Gaspar Kileo leo 18 Agosti 2026meongoza timu ya Wajumbe wa Mradi huo pamoja na Mshauri Mwelekezi Kutoka TBA na mkadarasi wa mradi Kufanya ukaguzi na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Utawala la Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dodoma.
Ukaguzi wa mradi huo unalenga kutathmini maendeleo ya ujenzi, ubora wa kazi zinazotekelezwa, kuzingatia michoro na viwango vya ujenzi, pamoja na utekelezaji wa mradi kwa kuzingatia muda na gharama zilizopangwa.
Mradi wa ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Idara ni miongoni mwa hatua muhimu katika kuimarisha mazingira ya utendaji wa Idara na kuwezesha watumishi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Katika ukaguzi huo, timu ya wataalamu imefanya tathmini ya hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi na kubaini maeneo yanayohitaji maboresho ili kuhakikisha kazi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa.
Ujenzi wa jengo hilo una umuhimu mkubwa kwa Idara ambayo ina jukumu la kusimamia utunzaji, uhifadhi na usimamizi wa kumbukumbu na nyaraka za Serikali.
Uongozi wa Idara unaendelea kusisitiza umuhimu wa kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa ubora, kwa kuzingatia thamani ya fedha na kwa wakati, ili kukamilika kwa jengo hilo kuwezeshe Idara kuwa na mazingira bora zaidi ya kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Taifa.
