Habari
MKURUGENZI SALAMA: WATUMISHI WAJITUME KULINDA NA KUENDELEZA TAASISI ZAO
MKURUGENZI SALAMA: WATUMISHI WAJITUME KULINDA NA KUENDELEZA TAASISI ZAO
Na Adeladius Makwega, OR-IKNT– DODOMA
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka, Bi. Salama Said Mohammed, amesema kila mtumishi wa umma ana wajibu wa kuonesha umahiri wake kazini ili kuhakikisha idara, kitengo na taasisi yake inakuwa taa inayong’aa vizuri kwa jamii ya Watanzania.
Hayo yamesemwa Agosti 17, 2026, wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa taasisi hiyo ofisini kwake.
“Unachopaswa kufanya unapofika katika taasisi ni kuangalia mpango kazi wa taasisi, kisha uangalie kile unachopaswa kufanya kwa kuzingatia miongozo ya taasisi, kanuni na sheria. Kisha fanya kazi kwa juhudi na kujituma ili kuhakikisha taasisi yako inasonga mbele,” alisema Bi. Salama.
Aidha, amesema kila mtumishi ana wajibu wa kufanya kazi bila kuchoka ili kuwatumikia wananchi wa Tanzania, kama anavyosisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wakati hayo yakizungumzwa, hali ya hewa ya Jiji la Dodoma mchana wa Agosti 17, 2026 ilikuwa na joto la nyuzi 26 Selsiasi, unyevunyevu wa asilimia 42, uwezekano wa mvua ukiwa asilimia 10, huku upepo ukivuma kwa kasi ya kilomita 13 kwa saa
