Tanzania emblem

Ofisi ya Rais

Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Building photo

Habari

WATENDAJI WAKUU WAHIMIZWA KUWEKA MKAZO KWA WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO


WATENDAJI WAKUU WAHIMIZWA KUWEKA MKAZO KWA WATUMISHI WA UMMA KUSHIRIKI KWENYE MICHEZO

 

Na OR-IKNT

Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, amewapongeza watumishi wa umma  waliojitokeza kwenye ufunguzi wa Bonanza na kuwahimiza watendaji wa kuu kuweka mkazo kwa watumishi wa umma kushiriki kwenye michezo.

 

Bw. Juma Mkomi ametoa pongezi hizo Agosti 15, 2026, jijini Dodoma, wakati watumishi wa umma kutoka taasisi mbalimbali waliposhiriki Bonanza Maalumu la Michezo lililoandaliwa kuelekea Michezo ya Watumishi wa Umma (SHIMIWI) 2026.

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bonanza hilo kwa niaba ya Katibu Mkuu Kiongozi, amesema Serikali inaendelea kuhimiza ushiriki wa watumishi katika michezo ili kujenga mshikamano, mahusiano mazuri na kuongeza tija katika maeneo ya kazi.

 

Amesema michezo inatoa fursa kwa watumishi kujenga mahusiano mema ndani na nje ya taasisi, jambo linalochangia kuimarisha ushirikiano na hatimaye kuongeza ufanisi katika kazi utekelezaji wa majukumu ya Serikali.

 

“Michezo inapofanyika inasaidia kujenga mahusiano mazuri baina ya watumishi ndani na nje ya taasisi. Mahusiano haya yanaweza kujenga ushirikiano mzuri na kuongeza tija katika kazi. Utumishi wa Umma unalenga kumhudumia na kumfikia Mtanzania kuanzia ngazi ya kitongoji na kijiji, kata, wilaya, mkoa hadi taifa,” alisema ndugu Mkomi.

 

Aidha, ndugu Mkomi aliwataka Wakurugenzi na Maafisa Rasilimali Watu katika taasisi za umma nchini kuhakikisha watumishi wanapewa nafasi na mazingira bora ya kushiriki katika michezo.

“Ninaagiza watumishi wa umma wapewe nafasi ya kushiriki michezo. Vilevile, watumishi wa umma wanapaswa kujiepusha na vitendo vya ulevi na mambo mengine yasiyofaa kwa jamii,” alisisitiza.

 

Pia amewataka Wakurugenzi na Maafisa Rasilimali Watu nchini kujenga utamaduni wa michezo katika taasisi zao kwa kuhakikisha watumishi wanapatiwa vifaa na fursa za kutosha kushiriki shughuli za michezo.