Habari
TRAMPA YATAMBUA MCHANGO WA MKURUGENZI WA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
TRAMPA YATAMBUA MCHANGO WA MKURUGENZI WA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA
DODOMA: Mkutano wa 14 wa Chama cha Wataalamu wa Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA), unaofanyika jijini Dodoma, umetambua mchango wa Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Firimin Msiangi, katika maendeleo ya kada ya Kumbukumbu na Nyaraka nchini Tanzania.
Katika hafla hiyo iliyofanyika mapema Septemba 23, 2026, TRAMPA ilimkabidhi Msiangi zawadi maalumu ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi na mchango wake wa muda mrefu katika kada hiyo.
Wakati akisoma maelezo ya zawadi hiyo, mwakilishi wa TRAMPA alisema Msiangi ni miongoni mwa wadau ambao mchango wao umetambuliwa na kuheshimiwa na chama hicho.
“Mkurugenzi Msiangi ni miongoni mwa wadau ambao mchango wao unatambuliwa na kuheshimika na TRAMPA. Mchango huu ni wa miaka mingi ukiwa ni mchango uliotukuka,” alisema.
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hiyo,
“Ninawashukuru wana TRAMPA kwa kutambua mchango wangu. Huku ni kutambua pia mchango wa Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa. Asanteni TRAMPA,” alisema Msiangi.
Mkutano wa 14 wa TRAMPA unafanyika jijini Dodoma na umefunguliwa Septemba 23, 2026, na Waziri wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete.
