Habari
KYANDO URGES FRAUD RISK MANAGEMENT COMMITTEE MEMBERS TO USE THE OPPORTUNITY TO GAIN DEEPER UNDERSTANDING OF THE INSTITUTION
KYANDO AWASISITIZA WAJUMBE WA UDHIBITI WA HATARI ZA UDANGANYIFU KUITUMIA FURSA HIYO KUIFAHAMU TAASISI
Na OR-IKNT
DODOMA, NOVEMBA 2, 2026
Mkurugenzi wa Idara ya Waasisi wa Taifa, Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Bw. Salum Kyando, amewasisitiza wajumbe wa Udhibiti wa Hatari za Udanganyifu kuitumia fursa hiyo kama nyenzo muhimu ya kujifunza, kuongeza uelewa na kuifahamu kwa kina taasisi, ikiwemo majukumu, mifumo na taratibu zake za kiutendaji.
Kyando amesema hayo. Wakati akifungua kikao kazi cha kuandaa andiko la Udhibiti wa Hatari za Udanganyifu kwa wajumbe walioteuliwa kufanya hivyo kuwa ni fursa ya kujenga uelewa mpana kuhusu taasisi na kuimarisha uwezo wa kutambua, kuzuia na kudhibiti vihatarishi vinavyoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
Aidha, amewahimiza wajumbe kuwa na ushirikiano, uwajibikaji na weledi katika mafunzo hayo ili kuhakikisha mifumo ya udhibiti wa udanganyifu inakuwa imara na inachangia ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi.
Amesisitiza kuwa uelewa wa pamoja kuhusu taasisi ni msingi muhimu katika kuimarisha uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za umma.
