Tanzania emblem

Ofisi ya Rais

Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Building photo

Habari

Ziara ya mafunzo ya Viongozi toka Kurugenzi Kuu ya Nyaraka za Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria


Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, yatembelewa na Viongozi toka Kurugenzi Kuu ya Nyaraka za Taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria. Ziara hiyo ya mafunzo kwa Viongozi hao ni utekelezaji wa Hati ya Makubaliano (MoU) katika fani ya nyaraka ambapo Nchi hizi mbili ziliingia Mwezi Agosti, 2023

 

Ugeni huo wa Viongozi wanne uliongozwa na Bw. Rida Ben Laksira, Mkurugenzi wa Uendelezaji Nyaraka Kidigitali. Waliweza kutembelea Ofisi zetu za Kanda ya Mashariki Dar es Salaam pamoja na Makao Makuu Dodoma. Pia walipata fursa ya kujifunza katika Makumbusho ya Taifa, Kituo cha Urithi wa Ukombozi wa Afrika pamoja na Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar