Habari
PERMANENT SECRETARY MKOMI EMPHASIZES THE IMPORTANCE OF MONITORING AND EVALUATION IN WORK PERFORMANCE
KATIBU MKUU MKOMI AMESISITIZA UMUHIMU WA UFUATILIAJI NA TATHMINI KATIKA UTENDAJI WA KAZI
Na OR-IKNT
DODOMA, 01 SEPTEMBA, 2026
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Mkomi, amesisitiza umuhimu wa ufuatiliaji na tathmini katika kuongeza ufanisi, uwajibikaji na kuhakikisha mipango ya Serikali inatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia viwango bora vya utendaji.
Bw. Mkomi ameyasema hayo leo, Septemba 01, 2026, wakati akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Ufuatiliaji na Tathmini kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, kamati ilijadili utekelezaji wa majukumu ya Ofisi kwa Robo ya Nne ya Mwaka wa Fedha.
Amesema taarifa za ufuatiliaji na tathmini zinapaswa kuwa msingi wa kufanya maboresho na maamuzi yanayozingatia ushahidi, na siyo kwa ajili ya kuonesha kiwango cha utekelezaji pekee.
Aidha, amewataka viongozi na watendaji kuzingatia matumizi bora ya rasilimali, uwajibikaji na utoaji wa huduma zenye tija kwa wananchi.
Kikao hicho kimewakutanisha wakuu mbalimbali wa taasisi zilizochini ya Ofisi ya Rais – Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa Bw. Firimin Msiangi.
