Tanzania emblem

Ofisi ya Rais

Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

Building photo

Matangazo

TANGAZO LA MNADA WA HADHARA


Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa inapenda kuwaalika wananchi wote kwenye mnada wa hadhara wa vifaa chakavu vya Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa.

Mnada utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 21/06/2025 kuanzia saa nne kamili (04.00) asubuhi katika eneo la Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa zilizoko Mtaa wa Vijibweni kata ya Upanga, nyuma ya jengo la Viva Tower, Dar es Salaam.

Wananchi wanaruhusiwa kukagua vifaa vitakavyouzwa kuanzia tarehe 19 Juni 2025 kuanzia saa 04:00 Asubuhi mpaka 08:00 Mchana.

VIFAA VITAKAVYOUZWA

Vifaa vitakavyouzwa ni pamoja na samani za ofisi, Bajaji, vifaa vya ujenzi, water dispenser, vifaa vya TEHAMA n.k

MASHARTI YA MNADA

1. Mnunuzi atatakiwa kulipa asilimia mia moja ya bei ya kifaa atakachonunua papo hapo siku ya mnada;

2. Mnunuzi atatakiwa kuhamisha kifaa atakachonunua ndani ya siku moja (1) baada ya mnada kufanyika;

3. Mali zote zitauzwa kama zilivyo na mahali zilipo.

Nyote Mnakaribishwa.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Ofisi ya Rais, Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa

29 Mei, 2025