Matangazo
Taarifa kwa Umma, Makao makuu ya Ofisi ya Rais,Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa kuhamia Dodoma.
Mkurugenzi,Ofisi ya Rais,Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa anautangazia Umma kwamba Makao makuu ya Idara, yatahamia rasmi Dodoma tarehe 15/07/2021,Hivyo huduma zote za kiutendaji zitakuwa ofisi za Dodoma-Barabara ya Swaswa na Ofisi za Dar Es Salaam zitabaki kuwa kituo cha Kumbukumbu Kanda ya Mashariki na Pwani.